Inasemekana ni kijana mrefu kuliko wote Tanzania. Kijana huyu
(katikati
pichani) ambaye anadhaniwa ni mrefu kuliko vijana wote
Tanzania anaishi
maeneo ya Gongolamboto, Banana jijini Dar es salaam.
Kijana huyu huwa haonekani sana mitaani, lakini aliingia mjini siku hiyo
na kuleta kizaa zaa kikubwa pale alipoibuka mitaa ya Aggrey, Kariakoo.
Alikuwa kivutio kwa kila aliyemuona, alifunga mtaa watu wakimshangaa
na
kumgombania kupiga nae picha. Kila aliyetaka kupiga nae picha alitoa
Shilingi elfu moja Tsh. 1000.
Picha hiyo amepigwa ndani ya Kinyozi (Salon) aliyoingia kupunguza nywele
zake na umati wa watu walikuwa nje ya kinyozi huyo kumsubiri atoke.
Mpaka sasa hajajulikana jina lake kamili na anafanya nini. Inasemekana
kuna watu wanamfuatilia kumsaidia umaarufu.
Ukimuangalia kwa mara ya kwanza mchezaji wa Tanzania anayecheza
timu ya
kikapu ya Oklahoma City Sounders inayoshiriki Ligi ya Kikapu
Marekani
(NBA), Hasheem Thabit unaweza kujiridhisha kwamba ni mrefu
kuliko
Watanzania wote uliowahi kuwaona. Ana futi 7.3.
Lakini mjini Bagamoyo katika Mkoa wa Pwani kwenye shule ya Lord Barden
yupo mchezaji anayemzidi Hasheem kwa urefu akiwa na futi 7.5.
No comments:
Post a Comment