Msanii nguli wa hip hop nchini Fid Q amefunguka na kusema kuwa yeye
hupenda kufanya kazi na wasanii wengine ambao pengine hawana majina
kwa wakati huo kwa sababu huamini zaidi kwenye kipaji kuliko jina.
Fid Q ameyafunguka hayo baada ya kuulizwa kwanini kwenye nyimbo zak
e nyingi hafanyi na watu wenye majina makubwa mfano Walk it off ambayo
amefanya na producer Taz tokea Zambia ambaye ni mpya masikioni mwa
watanzania wengi“mara nyingi mimi hupenda kufanya kazi na watu wasiofahamika
kwa sababu naamini kwenye talent zaidi kuliko majina,naamini kwenye kutengeneza nyimbo
nzuri kuliko hit song.” alifunguka Fid Q ambaye alisema hapendi kufuata trend bali hutengeneza
trend.
Source:Clouds
No comments:
Post a Comment