Mzungu Kichaa ametoa maoni yake kwa kusema ‘sikutegemea kwamba wimbo wa Nay wa Mitego ungefungiwa, ameongea vitu vya maana… anaongea kuhusu msumeno usiong’ata, pale anawalenga BASATA moja kwa moja lakini ni kitu ambacho inabidi BASATA wawe tayari kukichukua, wasione ni kitu kibaya… hiyo iwe mwanzo wa mazungumzo kujadili kitu, wasifungie tu wimbo‘
‘Napinga kuleta Upolisi kwenye sanaa kama hivi…. mi nimeupenda sana wimbo wa ‘shika adabu yako’ na nilikwenda kusoma mashairi kwanza kabla hata ya kuusikiliza wimbo, sio kwamba nakubali kila alichoandika pale ila ni vizuri kuwa na msimamo na kuongea kitu kinachotokea kwenye jamii ili tukijadili hata kama amesema kitu kibaya’ – Mzungu Kichaa
No comments:
Post a Comment