nishati na maji nchini (EWURA) ilitangaza bei
mpya ya bidhaa za mafuta ya Petrol, Diesel na
ya mafuta ya taa katika masoko yote ya jumla na
rejareja ambapo bei hizo zitaanza kutumika kuanzia
tarehe 2 march 2016.
Akiongea na waandishi wa habari Dar es salaam,
Mkurugenzi wa huduma za nishati na maji (EWURA),
Felix Ngamlagosi amesema ‘kuanzia tarehe 2 March
bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo
lililopita la February 2016, kwa March 2016 bei ya
rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa
na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na
7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa
lita sawa na 13.75%’
‘kwa kiasi kikubwa , kupungua huku kwa bei za mafuta
kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka
kwa bei za mafuta katika soko la dunia‘
No comments:
Post a Comment