Hii ni
dunia ambayo kila siku kuna watu wanafanya utafiti wa vitu duniani…
sasa
leo March 4 2016 nakuletea matokeo ya utafiti uliofanywa kwenye
bara la
Afrika na kuonyesha kwamba ifuatayo ndio miji kumi ya nchi za
Afrika
ambako Matajiri wengi wanapatikana.
Kila
tajiri aliejumuishwa kwenye hii list ni yule aliye na utajiri unaozidi
dola
za kimarekani milioni 30 ambazo kwa Tanzania ni zaidi ya BILIONI 65
ambapo moja ya miji hiyo 10 Dar es salaam ipo pia ikiwa nafasi ya sita
ikiwa na matajiri 36 wenye utajiri huo.
List kamili kwenye nafasi ya kumi ni mji wa 10. Kano Nigeria,
9– Marrakesh Morocco 8– Addid Ababa Ethiopia 7– Abuja Nigeria
6– Dar es salaam Tanzania 5– Nairobi Kenya ambako kuna matajiri
wa aina hiyo wapatao 69. Namba 4 ni Capetown South Africa yenye
matajiri 115 wa aina hiyo. 3- Lagos Nigeria yenye 131 2- Cairo Egypt
1. Johannesburg South Africa yenye matajiri wa aina hiyo 238.