Popular Posts

Sunday, February 28, 2016

Al Shabab yawaua 24 wakitizama Man U-Arsenal

Watu 24 wameuawa mjini Baidoa Kusini mwa Somalia wakitizama mechi baina ya Manchester United na Arsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na Al Shabab.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa milipuko miwili mikubwa ilitokea, katika
 mkahawa huo uliokuwa umejaa mashabiki wa mechi kati ya Manchester United
 na Arsenal.
Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo.
Mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji waislamu wa Al-Shabaab mwaka wa 2008,
 lakini walitimuliwa mwaka 2012.
Mji huo ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu ni mji wa hivi
 punde zaidi kushambuliwa na wanamgambo hao wa kiislamu.
Shambulizi la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na
 viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa bomu.


Walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa muungano wa Afrika AMISOM.
Shambulizi hili limetokea muda mchache tu baada ya kukamilika kwa warsha
 ya viongozi wa mataifa yanayochangia wanajeshi wake katika jeshi la muungano
 wa Afrika AMISOM.
Siku ya ijumaa watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika mgahawa mwengine
 kufuatia shambulizi la Al Shabaab.
 

No comments:

Post a Comment